Binti wa Chifu

Nitakupenda kikamilifu
ewe binti wa chifu.
Nitakutunza kama yai
bora afya na uhai.

Nitakutuza kikamilifu,
kilasiku ntakusifu;
chochote utakacho
nitakupa nipatapo.

Utanipenda kikamilifu
ewe binti wa chifu?
Utanitunza kama yai
bora afya na uhai?

Utanituza kikamilifu
kunisifu kilasiku?
Chochote nitakacho
utanipa upatapo?

Nipe nami nkupe,
nipende, ‘sinitupe!
‘Shasema yangu siri,
nistiri nikustiri.

Nistiri nikustiri,
nipe penzi nilivae
Ni wewe nimtakaye
Wewe tu unifaaye!

bintiwachifu

Advertisements
This entry was posted in Africa.

2 comments on “Binti wa Chifu

  1. Sonya Kassam says:

    Wow this is lovely! Though I had to get some help in translating. And the image is gorgeous.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s