Binti wa Chifu

Nitakupenda kikamilifu
ewe binti wa chifu.
Nitakutunza kama yai
bora afya na uhai.

Nitakutuza kikamilifu,
kilasiku ntakusifu;
chochote utakacho
nitakupa nipatapo.

Utanipenda kikamilifu
ewe binti wa chifu?
Utanitunza kama yai
bora afya na uhai?

Utanituza kikamilifu
kunisifu kilasiku?
Chochote nitakacho
utanipa upatapo?

Nipe nami nkupe,
nipende, ‘sinitupe!
‘Shasema yangu siri,
nistiri nikustiri.

Nistiri nikustiri,
nipe penzi nilivae
Ni wewe nimtakaye
Wewe tu unifaaye!

bintiwachifu