Lugha za Kiasili

Kuongea na kuelewa lugha tofauti tofauti ni jambo muhimu sana linaloweza kukupa uwezo wa kuelewa mila, dini na taaluma za kila aina. Lakini kabla ya kuelewa lugha zengine, ni muhimu kuielewa na kuihifadhi lugha yako ya kitamaduni, yeyote ile.

Lugha zetu za kiasili, haswa za Kiafrika ziko hatarini.Tusipochunga, zitasahaulika na kupotea. Tukipoteza lugha zetu, tutapoteza tarikhi zetu na mila zetu.

Nawaonea wivu wale wanaojua lugha mbili au zaidi za kiasili. Mimi najua moja tu, Kiswahili. Na nitailinda hiyo lugha moja sana sana.

Angalia Aborijini wa Australia na Wahindi wa Marekani. Wengi wao wamepoteza lugha zao. Tukiendelea tuendavyo, na sisi tutapatwa na yaliyowapata.

Lakini waangalie Wachina na Wajapani. Wameendeleza nchi zao sana licha ya kutumia lugha zao za kiasili.

Utapata watu wanajigamba kwa umaarufu wa lugha zisizo za kiasili. Lugha isiyo ya kiasili ni kama nguo ya kuazima. Usipochunga, mwenyewe atairudia nguo yake akuwache uchi.

Lugha ya kiasili ni lugha inayowakilisha uhuru wako na asili yako.

Tusisitesite kuongea lugha zetu za kiasili. Tujivunie uafrika wetu kwa kuimarisha uongeaji wa lugha za kiasili.

Kwahivyo, ongea lugha yako ya kiasili bila haya kwasababu kuimarisha lugha ya kiasili ni kuihakikisha uhuru wako.

african languages

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s